Animal
Monday, 29 February 2016
HISTORIA FUPI KUHUSU NYATI
Nyati ni mnyama mkubwa. Ana mita 1.7 juu, urefu wa mita 3.4. Nyati wa savana ana uzito wa kilo 500–900, ambapo nyati wa kiume kwa kawaida huwa mkubwa kuliko nyati wa kike, akiwa na uzito wa juu mbalimbali. nyati wa mwitu huwa na nusu wa kiwango hicho. Nyati wa savana huwa wa rangi nyeusi au kahawia nyeusi na pembe zao zimejikunja katika mpevu; nyati wa msitu nao huwa wa rangi ya kahawia nyekundu na pembe zao zimejikunja nyuma na juu. Ndama wa aina zote mbili wana ngozi nyekundu.
PICHA MBALIMBALI KUHUSU NYATI
HISTORIA FUPI KUHUSU SIMBA
Simba ni wanyama wenye nguvu ambao mara zote huwinda kwa makundi na kumkazania windo walilochagua. Hata hivyo hawajulikani sana kwa stamina yao, kwa mfano, moyo wa simba jike unajumisha tu asilimia 0.57 ya uzito wa mwili wake ( wa dume ni asilimia 0.45 ya uzito wa mwili wake), wakati ule wa fisi ni karibu na asilimia moja ya uzito wake. Hivyo basi japokuwa simba anaweza kufikia mwendokasi wa km 81 kwa saa, wanaweza kufanya hivyo kwa mwendo mfupi tu na inawapasa kuwa karibu na mawindo kabla ya kuanza shambulio. Hutumia mwanya wa kupunguza uoni; kwa kufanya uwindaji sana nyakati za usiku
MIFANO MBALIMBALI KUHUSU SIMBA MNYAMA

TWIGA
Twiga ni mnyama mzuri ambaye Tanzania hutumia alama yake kama urithi wa Taifa.Twiga ni mnyama mrefu kuliko wote duniani.Ana miguu mirefu,shingo ndefu sana,ulimi mrefu na pembe fupi zilizo butu.Mwili wake una mabaka yenye rangi ya kikahawia-njano na kuzungukwa na rangi ya maziwa.
Mnyama huyu anapatikana katika nyika hususan sehemu zenye migunga pamoja na mikakaya,miti ambayo huifurahia sana na ni chakula chake kikuu.Twiga hana ushindani mkubwa wa chakula na wanyama wengine kwa vile yeye hula majani ya juu nchani wakati wanyama wengine hawafikii majani hayo.
Hifadhi ya Mikumi
Mikumi ni moja ya hifadhi mashuhuri na kubwa nchini Tanzania. Inapatikana katika Mkoa wa Morogoro.
Eneo kuu na muhimu katika hifadhi hii ni uwanda wa mafuriko pamoja na safu za milima ambazo zinapatikana ndani ya hifadhi hii.
Mbuga za wazi ndizo zinazoshamiri katika uwanda wa mafuriko na kuishia katika misitu ya miombo inayofunika mabonde yaliyo chini ya hifadhi.

Twiga ndani ya Hifadhi ya Mikumi
-Ndani ya hifadhi ya Mikumi kuna simba ambao huwa wanaonekana wakiwa katika himaya yao na mara nyingine wakiwa juu ya matawi ya miti ili kukwepa majimaji wakati mvua zinapototesha ardhi ambayo ina udongo wa mfinyanzi.
mfano wa wanyama wanaopatikana mikumi
-.
Subscribe to:
Posts (Atom)