Monday, 29 February 2016


HISTORIA FUPI KUHUSU NYATI

Nyati ni mnyama mkubwa. Ana mita 1.7 juu, urefu wa mita 3.4. Nyati wa savana ana uzito wa kilo 500–900, ambapo nyati wa kiume kwa kawaida huwa mkubwa kuliko nyati wa kike, akiwa na uzito wa juu mbalimbali. nyati wa mwitu huwa na nusu wa kiwango hicho. Nyati wa savana huwa wa rangi nyeusi au kahawia nyeusi na pembe zao zimejikunja katika mpevu; nyati wa msitu nao huwa wa rangi ya kahawia nyekundu na pembe zao zimejikunja nyuma na juu. Ndama wa aina zote mbili wana ngozi nyekundu.

PICHA MBALIMBALI KUHUSU NYATI

Image result for MAISHA YA MNYAMA NYATIImage result for MAISHA YA MNYAMA NYATI

No comments:

Post a Comment