Monday, 29 February 2016


Hifadhi ya Mikumi

Mikumi ni moja ya hifadhi mashuhuri na kubwa nchini Tanzania. Inapatikana katika Mkoa wa Morogoro.
Eneo kuu na muhimu katika hifadhi hii ni uwanda wa mafuriko pamoja na safu za milima ambazo zinapatikana ndani ya hifadhi hii.
Mbuga za wazi ndizo zinazoshamiri katika uwanda wa mafuriko na kuishia katika misitu ya miombo inayofunika mabonde yaliyo chini ya hifadhi.
Twiga ndani ya Hifadhi ya Mikumi
Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za mraba 3230 na ipo umbali wa kilometa 283 magharibi kwa Dar es Salaam. Aidha hifadhi hii iko kaskazini kwa mbuga ya Selouse na iko njiani unapoelekea katika hifadhi ya Udzungwa, Selouse na Ruaha kwa barabara kutoka Dar es Salaam.
-Ndani ya hifadhi ya Mikumi kuna simba ambao huwa wanaonekana wakiwa katika himaya yao na mara nyingine wakiwa juu ya matawi ya miti ili kukwepa majimaji wakati mvua zinapototesha ardhi ambayo ina udongo wa mfinyanzi.
mfano wa wanyama wanaopatikana mikumi
-.
Image result for PICTURE OF ANIMAL Image result for PICTURE OF ANIMAL

No comments:

Post a Comment