Monday, 29 February 2016

TWIGA



Twiga ni mnyama mzuri ambaye Tanzania hutumia alama yake kama urithi wa Taifa.Twiga ni mnyama mrefu kuliko wote duniani.Ana miguu mirefu,shingo ndefu sana,ulimi mrefu na pembe fupi zilizo butu.Mwili wake una mabaka yenye rangi ya kikahawia-njano na kuzungukwa na rangi ya maziwa.

Mnyama huyu anapatikana katika nyika hususan sehemu zenye migunga pamoja na mikakaya,miti ambayo huifurahia sana na ni chakula chake kikuu.Twiga hana ushindani mkubwa wa chakula na wanyama wengine kwa vile yeye hula majani ya juu nchani wakati wanyama wengine hawafikii majani hayo.

No comments:

Post a Comment